FAHAMU KUHUSU SHAMBULIO LA SEPTEMBER ELEVEN
Shambulio la 9/11, mwaka 2001, maarufu kama September ,11 attacks. Hili ndio shambulio la kigaidi liliouwa watu wengi kwa mara moja katika historia ya dunia ,watu 2,977 walikufa na zaidi ya 25,000 walijeruhiwa ikiwemo majereha madogo na ya muda mrefu kama ulemavu. Shambulizi lilitokea ndani ya nchi ya Marekani, katika majiji ya Newyork katika majengo mawili ya kibiashara maarufu kama Twins towers trade center katika mtaa wa Manhattan, Virginia, Arlington katika jengo la Pentagon, ofisi za Ulinzi za Marekani, na Kwenye viunga vya stony creek, Jimbo la Pennsylvania baada ya shambulio hilo lililopangwa kutekelezwa katika makao makuu ya serikali Washington DC kushindikana. Mashambulizi hayo yalifanywa na kundi la kigaidi la Al_qaeda chini ya Osama, ambalo lilihusisha ndege 4 za boengi 757 na 767, za mashirika ya american airlines na United airlines baada ya kutekwa na magaidi hao punde baada ya kutoka viwanjani. Mashambulizi yalitekelezwa asubuhi ya 2:46_4:28 , yalikuwa mashambulizi ...