UCHAMBUZI KUHUSU TOYOTA HARRIER


 

Toyota Harrier ilizinduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 1998 na ilikuwa moja ya SUV za awali zilizoletwa na Toyota. Ingawa ilianza kama SUV ndogo, ilijulikana kwa muundo wake wa kisasa na vipengele vya kifahari.

Toyota Harrier ina vizazi vinne.

Kizazi cha kwanza kilitengenezwa kuanzia mwaka 1998 mpaka 2003, kizazi cha pili kilitengenezwa mwaka 2003 mpaka 2013, kizazi cha tatu mwaka 2013 mpaka 2020 na kizazi cha nne kilianza mwaka 2020 mpaka sasa.

Katika baadhi ya masoko, Toyota Harrier ilikuwa inauzwa kama aina ya "Lexus RX" kwenye nchi zingine, kwani Lexus ni chapa ya kifahari ya Toyota.

Nitaongelea kuhusu Toyota Harrier ya mwaka 2010.

Toyota Harrier 2010 ilikuja na chaguzi nne za injini na zote ni petroli. Ambazo ni lita 2.4 injini ya 2AZ, lita 3.0 injini ya 1MZ, lita 3.3 injini ya 3MZ hybrid na lita 3.5 injini ya 3GR. Zote zikiwa na 5 speed automatic transmission, hakuna manual. Zina option ya 2WD au 4WD. Kuna option ya air suspension. 


Viwango vya Toyota Harrier 2010(Grades)

1. Toyota Harrier Grade G.

Hii model ya kawaida ambayo huja na alloy rim inchi 17, CD/Radio player isiyo na touchscreen, keystart, siti za vitambaa na ni siti za kurekebisha mwenyewe(manual seat), haina steering control. 

2. Toyota Harrier Grade G L package.

Hii huja na alloy rim inchi 17, DVD player ikiwa na touchscreen, keystart, siti za ngozi, siti za umeme, usukani unamultfunction control na ina option ya sunroof tatu juu.

3. Toyota Harrier Premium Alcantara. 

Hii hufanana na Toyota Harrier L package lakini tofauti yake ni huja na alloy rim ya inchi 18, nembo ya Alcantara kwa muonekano wa nje na sunroof option tatu.

Muonekano wa ndani.

Ndani inaukubwa wa kutosha wa kubeba watu watano. L package na Alcantara ni luxury sana ukikaa unahisi kama umepanda Lexus Rx. Kwa upande wa dereva legroom ipo vizuri sana na hata mtu mrefu hukaa bila shida. Upande wa nyuma siti ni pana na kubwa ukiweka na siti ya katikati, muonekano wa siti za nyuma ni comfortable tabu sana hata kipindi cha safari huwezi kuhisi uko bored. Ukiongeza na zile sunroof tatu hufanya gari kuwa na mzunguko wa hewa nzuri ndani.

Kwenye sehemu za kutunzia na kuweka vitu, kwenye upande wa dereva kuna cupholder mbili, kwenye milango pia kuna sehemu ya kuhifadhia vitu, kwenye sakafu kuna tray ya kuhifadhia, glovebox na cubby box. Upande wa nyuma kuna mifuko kwenye siti za mbele na kwenye milango.

Toyota Harrier ina boot ndogo ukilinganisha na mshindani wake Vanguard. Hii ni kutokana na roof zake zilizochongwa na nyembamba. Hata hivyo nafasi bado ni kubwa ya kubeba mizigo ya familia ya watu watano. Na kama itahitajika nafasi zaidi, siti za nyuma zinaweza kukunjwa. Boot yake ya umeme ni nzuri huweza kujifungua yenyewe.

Ina vitu vingine ni kama DVD player, navigation, dual zone, climatic control, camera ya nyuma, multifunction steering control, power tailgate, wood trim, tilt telescopic steering.

Kwenye usalama ina airbag 6, 3 seatbelt point, ABS, Traction Control, EBD.

Muonekano wa nje ni wa SUV(Sport Utility Vehicle). Ina muundo mzuri wa kuangalia, kama vile stability yake. Grade zote huja na alloy rim na fog light.

Matumizi ya mafuta ya Toyota Harrier 2010

Lita 2.4 hutumia lita 1 kwa wastani wa kilometer 11.5

Ina accelerate kutoka 0-100km/h kwa sekunde 10.5.

Lita 3.0 hutumia lita 1 kwa wastani wa kilometer 9.7

Ina accelerate kutoka 0-100km/h kwa sekunde 7.6.

Lita 3.3 hutumia lita 1 kwa wastani wa kilometer 18.0 kumbuka hii ni Hybrid.

Ina accelerate kutoka 0-100km/h kwa sekunde 7.0.

Lita 3.5 hutumia lita 1 kwa wastani wa kilometer 7.8.

Ina accelerate kutoka 0-100km/h kwa sekunde 6.4.

Full tank ya Toyota harrier 2010 ni lita 72 kwa ya kawaida na 65 kwa hybrid.


Utulivu barabarani.

Harrier imetulia barabarani japokua kwenye kona inalala kidogo ila sio swala la kusema labda ni kwa sababu ya uendeshaji ila ni nature ya body ilivyo. Kwenye off-road haina matatizo zana japokua kwenye sehemu za kuteleza sanasana 2WD hupoteza ustahimilivu kwa haraka sana lakini 4WD huweza kumudu hali hiyo upesi.

Parts nyingi za Harrier hushare na RAV4, Crown, Vellfire na Prado. Lakini sehemu za suspension model ya AIRS ni gharama sana na ni ngumu kupata. Kwaio kuwa makini itunze kama yai.


Tofauti ya Harrier na Lexus Rx:

• Injini ya Lexus Rx option yake inaanzia lita 3.0 wakati harrier inaanzia lita 2.4


• Lexus Rx ni nzito na ndefu kwenda njuu kuzidi harrier.


• Kutokea mwaka 2008 mpaka sasa Harrier na Lexus Rx hawachangii uzao(generation). Kwaio harrier 2010 na Lexus 2010 ni uzao tofauti na hazifanani.


• Lexus Rx ipo vizuri sana(better equipped).


• Lexus Rx ni grade ya kifahari tu(luxury) lakini harrier kuna luxury na kawaida.

#TOYOTA #Harrier #Lexus #review #car #carreview

Comments

Popular posts from this blog

eSIM revolution

KAZI NA UMUHIMU WA SNORKEL "MKONGA" KWENYE GARI

JIFUNZE KUHUSU TOYOTA PROBOX