KAZI NA UMUHIMU WA SNORKEL "MKONGA" KWENYE GARI


 Mara nyingi huwa tunakutana na magari kwa pembeni yamewekwa bomba moja ubavuni lakini hatufahamu maana ya bomba zile kuwekwa. Na mara nyingi kumekuwa na ubishani mara kwa mara kuhusu ilo bomba linaloonekana kwenye Toyota Landcruiser Hardtop. Leo nitakufafanulia kwa uchache kuhusu hilo bomba ubavuni.

Kwa lugha ya kitaalamu huitwa "SNORKEL" na huwekwa sana kwenye gari za Toyota LC au 4×4 pick up.

Snorkel huwekwa kwa sababu mbalimbali, inaweza kuwekwa kama kifaa kinachovutia au kuongeza uwezekano wa hewa kuingizwa ndani. Moja ya faida ya snorkel ni kuongeza ufanisi wa injini, kuongeza matumizi mazuri ya mafuta, na kupunguza maintainance ya air filter mara kwa mara.

Snorkel kwenye gari hupanua mfumo wa hewa kuingia ndani ya injini, na huwekwa juu karibu na roof ya gari. Kwenye sehemu za vumbi au off-road sanasana hizi 4WD hutimua vumbi sana. Snorkel imeewekwa ili kuingiza hewa safi na baridi ili kuifanya gari kupumua vizuri. Hewa inayotoka juu sio chafu sana ukilinganisha na hewa inayoingia kutokea chini kwenye usawa wa bonnet na kuingia kwenye injini. Kuongezwa kwa fender flares kwenye Toyota 4×4 Pick up au SUV pia huzuia matairi yasirushe  uchafu mwingi. Lakini kwenye barabara kavu au sehemu kavu bado hewa itakayotimuliwa itaingizwa ikiwa na chembechembe salama.

Note: Fender flares ni vile vizuizi ambavyo huwekwa kwenye matairi kuzuia yasirushe matope na baadhi ya uchafu mwingine.

Sio tu huingiza hewa chafu iliyochujwa kuja kwenye air filter, pia huzuia maji kuingia. Ukiwa unaendesha 4wheel kwenye sehemu zenye matope, mito, madimbwi n.k. maji huweza kupenya chini kwa chini na kuingia kupitia kwenye mfumo wa kawaida wa kuingizia hewa. Maji huweza kutengeneza njia kwa urahisi na kupenya kupitia air filter na kuingia kwenye injini kitu ambacho sio sawa, hivyo snorkel inawajibika katika kuyaondoa maji nje.

Usisite kutufollow kwenye kurasa yetu Mycar Tanzania like, comment na share ili uwe wa kwanza kupata update.

#Toyota #landcruiser #hardtop #snorkel #review #car

Comments

Popular posts from this blog

eSIM revolution

JIFUNZE KUHUSU TOYOTA PROBOX