FAHAMU KUHUSU "L" STICKER KWENYE GARI.

 

FAHAMU KUHUSU "L" STICKER KWENYE GARI.

Mtu yoyote anayeendesha gari anatakiwa awe ameenda shule kwa ajili ya udereva ili apate leseni. Ili kuwa dereva mzuri unatakiwa uwe umepitia masomo ya nadharia na vitendo  darasani kwa muda wa wiki tatu mpaka nne.

Tuongelee hizo sticker za L rangi nyekundu ambazo huwa tunaziona kwenye baadhi ya gari zimebandikwa mbele na nyuma lakini hatufahamu ni nini maana yake, na ni kwaajili gani na ni kwa watu gani.

Maana ya herufi L nyekundu ina maana zifuatazo:

1. Sticker nyekundu herufi L kwenye gari humaanisha Learner. Hii inamaanisha kwamba mtu anayeendesha hilo gari hana uzoefu wa kutosha wa kuendesha japokua amemaliza kozi yake ya udereva.

2. Hizi sticker hubandikwa mbele na nyuma kutoa ujumbe kwa gari zinakuja mbele na zinazomfuata nyuma kuwa wachukue tahadhari kuwa gari linaendeshwa na Learner.

3. Alama pia unamuonya dereva kutokulipita gari hilo lenye herufi L. Ikimaanisha kwamba dereva anatakiwa ajihakikishie kuwa hakuna gari linalokuja mbele ndio alipite.

MAKOSA AMBAYO LEARNER HUWEZA KUYAFANYA WAWAPO BARABARANI.

1. Huwa muda mwingine husahau kutoa ishara ya indicator ya kwenda kulia au kushoto.

2. Anaweza kujisahau na kuweka emergency brake katikati ya barabara kwa bahati mbaya.

3. Anaweza kuwa anahamahama mstari kwa bahati mbaya

NINI CHA KUFANYA UONAPO L STICKER KWENYE GARI.

1. Zingatia umbali kati yako na wewe usimsogelee sana(Keep distance)

2. Msiwapigie kelele wala kuwafokea maana mnaweza kuwachanganya na kufanya vitu visivyotarajiwa kama vile kukanyaga breki ghafla kwenye sehemu hatari.

3. Waelekeze pindi utakapoona wamekosea usiwanyooshee vidole na kuwatukana watakapokosea.

Tembelea kurasa yetu Mycar Tanzania like, comment na share ili uwe wa kwanza kupata update hizi.

#car #learnerdriver #review #egno2

Comments

Popular posts from this blog

eSIM revolution

KAZI NA UMUHIMU WA SNORKEL "MKONGA" KWENYE GARI

JIFUNZE KUHUSU TOYOTA PROBOX