TUJIFUNZE KIDOGO MAANA YA PLATE NAMBA NA RANGI ZAKE

 


TUJIFUNZE KIDOGO MAANA YA PLATE NAMBA NA RANGI ZAKE

1. Kibao chenye rangi ya njano na namba inayoanza na herufi T

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limesajiliwa kutumika kwa ajili ya shughuli binafsi. Kwa kiingereza inasemwa "private use". Magari yenye vibao hivi hayaruhusiwi kutumika kwa ajili ya biashara.

2. Kibao chenye rangi nyeupe na namba inayoanza na herufi T

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limesajiliwa kwa ajili ya matumizi ya biashara. Kwa kiingereza inasemwa "commercial use". Mfano mzuri daladala au basi za kubeba abiria na taxi.

3. Kibao chenye rangi ya njano na namba haianzi na herufi T

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na taasisi ya umma au serikali. Hapa kuna makundi yafuatayo:

(a) SU - shirika la umma , mfano vyuo vikuu vya serikali

(b) SM - Serikali za Mitaa , mfano ni halmashauri

(c) STK,STL,STJ - serikali, mfano ni wizara

4. Kibao chenye rangi nyekundu na namba inayoanza na herufi DFP au DFPA

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limetolewa kwa ajili ya matumizi ya miradi inayofadhiliwa na wafadhili kutoka nje ya nchi.

5. Kibao chenye rangi ya bluu na namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na moja ya shirika la umoja wa mataifa. Mfano shirika la Afya Duniani (WHO).

6. Kibao chenye rangi ya kijani na namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na ofisi za ubalozi wa nchi fulani. Mfano ubalozi wa Ufaransa.

7. Kibao chenye rangi nyeusi na namba zimeandiwa kwa rangi ya njano

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Polisi. Namba hizi huwa na herufi PT

8. Kibao chenye rangi nyeusi na namba zimeandiwa kwa rangi ya nyeupe

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Wananchi (JW). Namba hizi huwa na herufi JW.

9. Kibao chenye rangi ya kijani na namba zenye herufi MT

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Magereza.

Soma na ufahamu tofauti za namba zinazowekwa kwenye magari.

Usisite kutufollow kwenye kurasa Mycar Tanzania like comment na share ili uwe wa kwanza kupata update.

#tanzania #platenumber #knowledge

Comments

Popular posts from this blog

eSIM revolution

KAZI NA UMUHIMU WA SNORKEL "MKONGA" KWENYE GARI

JIFUNZE KUHUSU TOYOTA PROBOX