FAHAMU MATUMIZI YA GIA L, 2 NA 3 KATIKA GARI AUTOMATIC
FAHAMU MATUMIZI YA GIA L, 2 NA 3 KATIKA GARI AUTOMATIC Katika gari za Automatic kuna gia za L, 2, na 3. Watu wengi hawafahamu kiundani matumizi ya gia hizi hivyo mara nyingi hujikuta wanakosea wapi na namna ya kuzitumia. Katika maelezo haya hapa chini, tumekufafanulia namna ya kutumia gia hizo. Kwanza kabisa ujue katika hali ya kawaida gari lako linapaswa kuwa katika D (Drive) na hii inategemeana na mazingira ya barabara na hali ya hewa kama ni nzuri. Lakini 2, 3, hutumika tu pale unapokuwa aidha unateremka au unapanda mlima mkali na unataka ushuke au upande kwa spidi isiyozidi 40/60, hapo ndipo unaruhusiwa kutumia 2, na 3. Namba 2, 3 na L ina maana kuwa unalock giaboksi (gearbox) ili gia zisibadilike (+/-) kama ambavyo zinabadilika ukiweka D. Itambulike kuwa unaweza kubadili kutoka D kwenda 2 au 3 wakati wowote gari inapokuwa katika mwendo ila hakikisha usiwe katika mwendokasi wa zaidi ya 40/60. Maana kinachofanyika ni kwamba D inasababisha sahani (disk) zilizomo ndani ya gearbox kuf