HISTORIA YA ERWIN SCHRÖDINGER NA TAFITI ZAKE MAARUFU

 


Mmoja ya mdau aliomba ni muongelee erwin schrödinger katika chapisho lijalo" Athumani Juma"


•Erwin schrödinger alikuwa mwanafizikia maarufu wa Austria na mtaalamu wa nadharia ya quantum katika miaka ya 1920 na 1930 ,Alizaliwa mnamo Agosti tarehe 12 mwaka 1887 huko vienna Austria na alifariki mnamo januari 4 mwaka 1961 


•Moja ya mchango wake wa kipekee katika fizikia ni uundaji wa equation ya schrödinger ambayo ni msingi wa nadharia za quantum ,Equation hii inaweza kutabiri tabia ya chembe ndogo kama vile elektroni na imesaidia kufafanua sifa za kimwili za vifaa vya quantum.


•Licha ya umuhimu wake katika kukuza nadharia za quantum ,schrödinger anajulikana zaidi kwa ajili ya majaribio maarufu kama jaribio la paka la schrödinger 

Aliweza pokea Tuzo nobel ya fizikia mnamo 1933 kwa ugunduzi wake wa equation ya schrödinger 


Hizi ni gunduzi kazaa za erwin schrödinger


1.Wave mechanics:Schrödinger alitunga na kuendeleza mfumo wa equation za kibango za kugundua hali ya mwendo wa magimbi ya kvantamagimbi ,mfumo huu unajulikana kama equation ya schrödinger ilionyesha uwezo wake wa kutoka maelezo ya kiwango cha uwezekano wa kupata chembe (particula) kwenye eneo fulani 


•Schrödinger equation ambayo ni sheria msingi katika fizikia ya quantum ,schrödinger alibuni sheria hii mwaka 1925 kama njia ya kuelezea tabia ya mifumo ya quantum kama vile atomi na chembe ndogo ndogo 


Sheria hii ni equation ya kawaida ya kianuwai ambayo inaunganisha "wave function" inayowakilishwa na herufi ya kigiriki itwayo psi((Ψ) ni jukwa la hisabati ambalo linaelezea usambazaji wa uwezekano wa kupata chembe mahali fulani 


•Sheria ya schrödinger ilibadilisha uga wa mitambo ya quantum kwa kutoa mfumo wa hisabati unaowezesha kuchunguza tabia ya chembe katika kiwango cha quantum 

Ili ruhusu wanasayansi kufanya utabiri kuhusu viwango vya nishati ,mistari ya spektra ,na mali nyingine za atomi na molekuli ,ikirababisha uelewa wa kina wa ulimwengu mdogo


2.Schrödinger cat(tafiti ya paka):Katika makala yake ya kushangaza iliyo sadifu maswali ya mwingiliano kwenye ngazi ya subatomiki ,schrödinger alitunga hali ya kifikira ya paka aliye katika kuwa hai na kufa sawia 


•Fikiria hali ambapo paka amefungiwa kwenye chumba ,kuna sumaku yenye asilimia 50 ya kutoa radiesheni hatari ambayo inaweza kumua paka ,kulingana na nadharia ya quantum tumepewa uwezo wa kuwa katika hali zote mbili za radiesheni hatari na bila hatari wakati huohuo kwa maana hiyo paka anaweza kuwa hai au amekufa wakati huo huo ,schrödinger alitumia mfano huu wa paka ili kuelezea changamoto za kuunganisha nadharia ya quantum na maoni ya kawaida ya kimwili ,ni muhimu kuelewa kuwa mfano huo ni wa kufikirika 


•Pia aliweza uunda equation ,ambazo inafahamika kama schrödinger field equation ,na pia kuwa na mchango katika falsafa za fizikia 


Unaweza comment mwanasayansi unaempendekeza ni mzungumzie katika post ijayo,au topic(maada) yoyote ya kisaynsi ,nadharia yoyote ya kisayansi ,chochote kinacho uhusiana na maswala ya ang(unajimu)

Comments

Popular posts from this blog

eSIM revolution

KAZI NA UMUHIMU WA SNORKEL "MKONGA" KWENYE GARI

JIFUNZE KUHUSU TOYOTA PROBOX